Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA AFISA MTENDAJI MKUU WA TAASISI YA BWB YA UINGEREZA

19 Aug, 2024
DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA AFISA MTENDAJI MKUU WA TAASISI YA BWB YA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (katikati), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, uchumi na maendeleo ya kijamii, jijijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya BWB, Bw. Matteo Scalabrino.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo Afya, elimu, Uchumi na maendeleo ya kijamii.

Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika jijini Dodoma yamehudhuriwa na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justin, Mkurugenzi wa Taasisi ya BWB, Bw. Matteo Scalabrino na wajumbe wengine kutoka pande hizo mbili.