Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MPANGO AMUAGIZA WAZIRI WA FEDHA KUPITIA KODI YA MAJIKO

11 Mar, 2024
DKT. MPANGO AMUAGIZA WAZIRI WA FEDHA KUPITIA KODI YA MAJIKO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe) Dkt. Philip Isdor Mpango, akimsikiliza mmoja wa wadhamini (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuangalia uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia hasa kipindi hiki ambacho maandalizi ya bajeti ijayo yanafanyika.
 
Maagizo hayo ameyatoa wakati akifungua Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
 
Aidha Mhe. Mpango amezitaka Sekta Binafsi nchini kutumia fursa ya kutokomeza matumizi ya nishati chafu kama  njia moja wapo ya kuongeza kipato chao na kukuza uchumi wa nchi.
 
‘’Natoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono na kuchangia katika kampeni ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu. Baadhi ya maeneo ambayo sekta binafsi inaweza kusaidia ni kuwekeza katika utafiti, ubunifu na uzalishaji wa nishati safi na nafuu ya kupikia’’ alisema Mhe. Dkt. Mpango.
 
Aliongeza kuwa matumizi ya nishati chafu kama vile mkaa na kuni yameleta athari kubwa zaidi kiafya kwa wananchi hususani wanawake ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.
 
‘’Wanawake huvuta moshi mwingi wenye viwango vikubwa vya sumu, ambazo husababisha magonjwa ya mfumo wa hewa yanayosababisha vifo takriban 33,000 vya watanzania kila mwaka’’ alisisitiza Mhe. Dkt. Mpango.
 
Kongamano hilo limefanyika kama sehemu yakuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha wanawake kutumia nishati safi ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.  
 
Mwisho.