Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BI. OMOLO APONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE KWA UTOAJI WA ELIMU MAONESHO YA NANENANE DODOMA.

08 Aug, 2025
BI. OMOLO APONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE KWA UTOAJI WA ELIMU MAONESHO YA NANENANE DODOMA.

Naibu Katibu Mkuu (Huduma za Hazina), Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watumishi kutoka Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

 

Naibu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma ili kujionea huduma zinazotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake.

Bi. Omolo ameipongeza Wizara na Taasisi kwa kushiriki katika Maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “ChaguaViongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi2025’’, ili kufikisha elimu kwa wananchi hasa katika sekta ya kilimo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

‘‘Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha wananchi katika Maonesho haya hakika elimu mnayoitoa italeta tija katika utekelezaji wa majukumu ya wananchi ya kila siku hivyo kuchangia katika ukuaji wa sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na uchumi kwa ujumla’’, alisema Bi. Omolo.

Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake imetoa elimu kwa wananchi kuhusu Bajeti ya Serikali, Sera, uwekezaji, pensheni na mirathi, ununuzi wa umma na ugavi, masomo ya vyuo vya elimu ya juu, mifumo ya fedha, takwimu, rufaa za kodi, usuluhishi pamoja na huduma za kibenki.

MWISHO.