Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA UCHUMI IMARA

17 Oct, 2022
BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA UCHUMI IMARA

BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

 

Dkt. Nyamadzabo alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa uchumi ambapo licha ya majanga ikiwemo changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara na nchi inakopesheka.

 

Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia rasilimali fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Taufila Nyamadzabo kwamba uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua muhimu kuhakikisha uchumi unazidi kuimarika na kuleta ahueni kwa wananchi.

 

Alifafanua kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 uchumi umekua kwa asilimia 5.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.0 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa asiliia 6.3.

 

Aidha, Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alirejea shukrani zake kwa Benki ya Dunia kwa kuitengea Tanzania jumla ya dola za Marekani bilioni 2.1 sawa na shilingi trilioni 4.9 katika mzunguko wa 20 wa IDA (Julai 2022 – Juni 2025) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umasikini wa watu wake.

 

Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 7.2, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 16.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 29 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 24 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.41 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.75 ni ya kikanda.

 

Mwisho