Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BENKI YA DUNIA YAFADHILI MPANGO WA TAKWIMU TANZANIA

30 Jul, 2023
BENKI YA DUNIA YAFADHILI MPANGO WA TAKWIMU TANZANIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akifungua kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ya Pamoja ya Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini, yaani Tanzania Statistical Master Plan II, ambao unafadhiliwa kwa sehemu na mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Kimarekani milioni 82, chini ya Mpango wa Takwimu wa Kanda ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa katika nchi za Tanzania, Kenya na Rwanda. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
 
 
 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amesema kuwa Mfumo wa Kitaifa wa Takwimu unaofanya kazi kwa ufanisi, gharama nafuu na wenye uwezo wa kutoa takwimu bora na za uhakika utasaidia nchi kuweka mipango yake ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, wa mwaka 2020 - 2025 na maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa 2025 - 2030.
 
Dkt. Mwamba amesema hayo wakati akifungua kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ya Pamoja ya Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini, yaani Tanzania Statistical Master Plan II, Jijini Dar es Salaam.
 
Mpango Kabambe wa Pili wa Takwimu Nchini unafadhiliwa kwa sehemu na mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Kimarekani milioni 82, chini ya Mpango wa Takwimu wa Kanda ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa katika nchi za Tanzania, Kenya na Rwanda. 
 
Alisema kuwa katika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya takwimu na changamoto za upatikanaji wake, Serikali imekuwa ikichukua hatua za makusudi za kuimarisha uzalishaji wa takwimu nchini ukiwemo Mpango Kabambe wa Pili wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini, utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2022/23 hadi 2026/27. 
 
“Mpango huu unakusudiwa kudumisha na kuendeleza mafanikio ya Mpango Kabambe wa Kwanza wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu Nchini, yaani TSMP I kwenye vipengele vikuu vitatu vikiwemo Uratibu, Ubora na Usambazaji wa Takwimu; Uzalishaji wa Takwimu na Miundo ya kitaasisi na Miundombinu” Alisema Dkt. Mwamba
 
Alisema kuwa Serikali inatambua mchango na ushirikiano mkubwa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, sekta binafsi, wana taaluma, Asasi za Kiraia na wadau wengine katika kuimarisha Mfumo wa Kitaifa wa Takwimu nchini kupitia misaada yao ya kifedha na kiufundi na kwamba bado vitu hivyo vinahitajika katika safari ya kuimarisha takwimu nchini. 
 
“Nitumie fursa hii kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Mkutano huu na kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa shukrani zangu za dhati kwa Benki ya Dunia na Washirika wetu wote wa Maendeleo kwa misaada na ushirikiano wenu katika maendeleo ya takwimu Nchini.
 
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Katibu Mkuu, Ofisi Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Dkt. Juma Malik, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais-Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum, alisema Mpango huo wa kuboresha Takwimu utaisaidia Zanzibar kufikia malengo yake ya kukusanya Takwimu zitakazochangia upangaji wa maendeleo ya nchi.
 
Alisema kuwa Awamu ya kwanza ya Mpango huo, Zanzibar uliinufaika kwa kujengewa majengo mawili kama sehemu ya kuboresha miundombinu, na katika awamu ya pili, nchi yake itajengewa majengo mengine matatu.
 
Wakitoa maelezo ya Awali, Mtakwimu Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. Albina Chuwa na Mtakwimu Mkuu Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Salum Kassim Ali, walisema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri na kuonesha viwango vya juu vya ukusanyaji wa Takwimu na kwamba katika Awamu ya pili, Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 duniani zitakazonufaika na Mpango huo ambao wameahidi watausimamia vizuri ili kuhakikisha kuwa nchi inaboresha Takwimu.
 
Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, ambayo imetoa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 82 kwa ajili ya kutekeleza Mpango huo, Bi. Preeti Arora, alisema kuwa Mpango huo umelenga kuiwezesha Tanzania kuzalisha takwimu zenye ubora, na kuzisambaza kwa wakati ili ziwasaidie watunga sera kuweka mipango bora ya maendeleo.
 
Mwisho