Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA (TDB) YAISAIDIA TANZANIA KUPAMBANA NA UVIKO -19

17 Oct, 2022
BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA (TDB) YAISAIDIA TANZANIA KUPAMBANA NA UVIKO -19

Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika(The Eastern and Southern African Trade and Development Bank - TDB)  imeipatia Tanzania msaada wa Vifaa tiba vya Kujikinga na UVIKO -19 (PPE) vyenye thamani ya dola za Marekani 100,000 zaidi ya Shilingi milioni 238.

 

Akizungumza wakati akipokea msaada huo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amesema lengo la msaada huu, ni kuisaidia Serikali ya Tanzania kupitia Programu ya Dharura ya Kukabiliana na UVIKO-19 (TDB’s COVID-19 Emergence Response Programme - CERP) ili kununua PPE kwa ajili ya kuwakinga wahudumu wa afya dhidi ya maambukizi ya janga la UVIKO-19.

 

Mhe. Chande aliishukuru Benki ya TDB kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada huo na kuongeza kuwa janga la UVIKO-19 ingawa kwa sasa kasi ya maambukizi yake yamepungua lakini lilipunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya ukuaji wa uchumi, na kuathiri maisha ya watu duniani kote.

 

‘’Kama tunavyofahamu, Janga la UVIKO-19 limeleta athari katika masuala ya kiuchumi na kijamii kama vile usalama wa chakula, lishe, elimu, biashara na utalii, na hivyo kuhatarisha ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi yaliyokuwa yamepatikana’’. Alisema Mhe. Chande

 

Aidha, Mhe. Chande aliongeza kuwa pamoja na msaada huu, Benki ya TDB imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia miradi mbalimbali ya kimkakati katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini zikiwemo; sekta za miundombinu, nishati, viwanda, biashara ya kilimo pamoja na mafuta na gesi.

 

Awali akizungumza katika hala hiyo, Mtendaji wa Benki ya TDB wa Mahusiano na Uwekezaji Bi. Mary Kamari alisema Benki hiyo imeamua kutoa msaada huo kutokana na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Tanzania kama mwanahisa wa Benki hiyo. Aidha Bi.Kamari aliongeza kuwa TDB itaendelea kuchangia katika sekta mbalimbali za maendeleo za washirika wake ikiwemo Tanzania.

 

Pia Kamishina Msaidizi wa Idara ya Fedha za nje Wizara ya Fedha na Mipango Bw. James Msina alisema kuwa Serikali ya Jahmuri ya Muungano wa Tanzania ni mojawapo ya wanahisa wakubwa wanne (4) wenye hisa nyingi katka Benki ya TDB ambapo Tanzania ipo kwenye kundi la wanahisa daraja A.

 

Bw. Msina aliongeza kuwa Tanzania inanufaika kwa kiasi kikubwa na Benki hiyo kupitia mikopo ya Kibiashara na Maendeleo inayoipata kupitia TDB kwa upande wa Serikali na Sekta binafsi.

 

Mhe. Chande aliwahakikishia Watendaji wa Benki hiyo kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kushirikiana na TDB kwa maendeleo ya wananchi na kuitaka Benki hiyo kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mengine ya uchumi ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na uchumi imara na thabiti. Aidha Mhe. Chande alieleza kuwa msaada uliotolewa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.   

 

Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (The Eastern and Southern African Trade and Development Bank - TDB), inaundwa na nchi wanachama 23 kutoa katika nchi wanachama wa COMESA, SADC na EAC.

 

Mwisho