Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BALOZI OMAR: BARAZA LA MASOKO YA MITAJI LITOE ELIMU YA MAJUKUMU YAKE

21 Feb, 2026
BALOZI OMAR: BARAZA LA MASOKO YA MITAJI LITOE ELIMU YA MAJUKUMU YAKE

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, baada ya kumalizika kwa kikao kati yao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameitaka Mamlaka hiyo kutoa elimu kuhusu Baraza hilo ili wadau wengi waweze kulitumia kutatua changamoto zao.

Mhe. Balozi Omar, ametoa maelekezo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Baraza la Masoko ya Mitaji ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, alieleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuvutia mitaji na kukuza maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Baraza hilo ni kuwa na jukwaa maalumu kwa ajili ya usikilizwaji wa migogoro inayohusu Masoko ya Mitaji.

Alisema kuwa Baraza hilo lina Mamlaka pia ya kusikiliza migogoro inayotoka kwenye Soko la bidhaa yakiwemo masuala ya stakabadhi gharani.

Kikao hicho kimehudhuliwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Msajili wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Dkt. Martin Kolikoli na  Kaimu Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema.

Mwisho.