YALIYOJIRI SABASABA KATIKA BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Maafisa kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali (ACGEN), Bw. Almasi Chimodoi (kulia), Bi. Stellah Mtally (katikati) na Bi. Gillian Makule (kushoto), wakitoa elimu kuhusu utaratibu wa malipo ya mafao ya uzeeni na mirathi, namna ya uwasilishaji michango ya watumishi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, pamoja na uratibu na usimamizi wa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, kwa wananchi waliyotembea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.