WIZARA YA FEDHA YATOA WITO KWA WATUMISHI KUJITAYARISHA KWA MAISHA BAADA YA KUSTAAFU

Watumishi wa Wizara ya Fedha wametakiwa kuanza kujiandaa mapema kwa maisha ya baada ya kustaafu kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ili kuendelea kuwa na tija kwa familia na taifa hata baada ya kumaliza utumishi rasmi. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo, wakati akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu – Utawala, Bi. Jenifa Christian Omolo, katika hafla ya kuwaaga Waandishi Waendesha Ofisi waliostaafu, iliyofanyika katika Ukumbi wa Simba Hoteli jijini Dodoma.