WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA UCHAMBUZI WA BAJETI SEKTA YA UZALISHAJI
Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, inaendelea na uchambuzi wa bajeti ya sekta ya uzalishaji kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Sekta hiyo inajumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini.
Hatua hiyo inalenga kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti ya sekta muhimu za uzalishaji ili kuhakikisha yanazingatia vipaumbele vya Taifa, sera za maendeleo, mikakati ya kitaifa pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti.
