WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAWASHUKURU WAANDISHI WA HABARI
WIZARA ya Fedha na Mipango imesema inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma kusuhu Sera, Mipango, na Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na serikali kupitia wizara hiyo.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango.