WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAANZA KUWANOA WAJUMBE WA TIMU KUU ZA MAANDALIZI YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Timu Kuu za Uandishi na Uhariri wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuhakikisha zinakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu machakato wa maandalizi ya Dira hiyo. Warsha hiyo elekezi ya siku 4 inafanyika katika ukumbi wa PSSSF Golden Jubilee Tower, jijini Dar es Salaam.