WIZARA FEDHA YAPOKEA TUZO MBILI ZA USHINDI SHEREHE ZA MEI MOSI

Wizara ya Fedha imeng'ara kwenye Sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano yaliyoshirikisha Wizara na Taasisi za Serikali. Tuzo za washindi katika mashindano mbalimbali zimetolewa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.