WAZIRI WA FEDHA MHE. BALOZI OMAR: SEKTA YA BIMA NI MUHIMU KIUCHUMI NA KIJAMII

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Sekta ya Bima ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa, hususan katika kulinda mali na shughuli za kiuchumi za wananchi na taasisi. Mhe. Balozi Khamis amesema hayo Jijini Dar es salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ukiongozwa na Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo na mustakabali wa sekta ya bima nchini.