WAZIRI WA FEDHA BALOZI OMAR AISHAURI BENKI YA DUNIA KUIWEZESHA SEKTA BINAFSI
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, ameishauri Benki ya Dunia kuangalia namna ya kuiwezesha sekta binafsi katika nchi za Afrika ili iweze kuwa imara na kuchangia kukuza uchumi wa nchi hizo.
Mhe. Balozi Omar, ametoa wito huo wakati akichangia mada katika mkutano wa Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika, wanachama wa Benki ya Dunia (Africa Group 1 Constituency), uliofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
