WAZIRI WA FEDHA AZINDUA MKUTANO WA MAPITIO YA SEKTA YA MAJI, ATAKA USHIRIKIANO KUIMARISHA HUDUMA NCHINI
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amezindua rasmi Mkutano wa Mapitio ya Pamoja ya Sekta ya Maji (Joint Water Sector Review) na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watanzania wote.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Cate Convention Centre, Morogoro, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa sekta ya maji ni mhimili muhimu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na hivyo inahitaji uwekezaji endelevu na usimamizi madhubuti wa rasilimali za maji.
