WAZIRI WA FEDHA ATETA NA MABALOZI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Mhe. Marianne Young pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Waziri alisisitiza dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuimarisha sekta mbalimbali, hususan zile zinazogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.