WAZIRI WA FEDHA AITAKA TRA KUCHANGIA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, ijipange ipasavyo kuhakikisha kuwa inachangia upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo imeainisha kuwa na uwiano wa Pato la Taifa wa shilingi trilioni 1 ifikapo mwaka 2050. Mhe. Balozi Omar alisema hayo alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TRA wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka hiyo, ikiwa na mara yake ya kwanza Tangu ateuliwe na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya MUuungano wa Tanzania kushika wadhifa huo hivi karibuni. Alisema kuwa Dira iliyomaliza muda wake iliitaka Tanzania kufikisha uwiano wa Pato la Taifa wa dola za Marekani bilioni 90 hadi kufikia mwaka 2025 lakini makadirio mapya yanataka kiwango hicho kifikie dola za Marekani trilioni 1 ambazo TRA inatakiwa kujipanga ipasavyo kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kiwango cha asilimia 70 ili kutekeleza Dira hiyo ipasavyo.