WAZIRI WA FEDHA AIPONGEZA TRA KWA UTENDAJI MZURI WA MAKUSANYO YA MAPATO

Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (MB), ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, hatua iliyochangia kuimarika kwa uchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Ametoa Pongezi hizo wakati akifungua Mkutano wa Kutathmini Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Nusu Mwaka wa Fedha 2025/26 (Mid-Year Performance Review Meeting), uliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.