WAZIRI WA FEDHA AAHIDI USHIRIKIANO ILI KUFIKIA MALENGO YA KUKUZA UCHUMI WA NCHI NA MAENDELEO YA JAMII
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Wizara ya Fedha imebeba matumaini ya Serikali na Wananchi katika kuhakikisha kuwa inatafuta fedha za kuendeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi.
Mhe. Balozi Omar, amesema hayo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Wizara ya Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Menejimenti na Wafanyakazi wa Wizara hiyo, baada ya kuwasili katika Ofisi hizo akiambatana na Naibu Mawaziri wake wawili, Mhe. Mshamu Ali Munde na Mhe. Laurent Deogratius Luswetula.
