WAZAWA WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MIRADI YA AfDB

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuangalia uwezekano wa kuboresha Sheria yake ya Ununuzi ili miradi inayotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo iweze kuwanufaisha wakandarasi wa ndani. Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo jijini Dodoma wakati wa mkutano kati yake na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya AfDB nchini Tanzania, Bi. Patricia Laverley, uliofanyika kwa njia ya mtandao ambao umeangazia namna bora ya kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo.