WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WATAKIWA KUENDELEA KUZINGATIA SHERIA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amewataka watumishi wa wizara hiyo kuendelea kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ili kumuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta mageuzi na mabadiliko ya kiuchumi nchini. Dkt. Mwamba alitoa rai hiyo wakati akifungua mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.