WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WAHITIMISHA TAMASHA LA PASAKA

Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na MipangoZanzibar kwa Mwaka 2024, limehitimishwa baada ya watumishi wa Wizara ya Fedha pande zote mbili za Muungano kukamilisha zoezi la kutoa misaada kwa vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji maalum na vituo vya watoto yatima. Akizungumza katika hafla ya kuagana na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa’ Golden Crown’ jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, aliwashukuru watumishi wote wa pande zote mbili kwa ushiriki wao katika Tamasha hilo huku akiahidi kufanyika kwa tukio kama hilo mwakani.