WATAALAMU WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN WACHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA
Tanzania imetambua na kuthamini mchango wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kwa kipindi cha miaka 60.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanza kwa mpango wa kuleta wataalamu wa kujitolea kutoka Japan nchini Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
