WATAALAM WANAOSIMAMIA UAANDAAJI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI WAASWA KUTUMIA KIKAMILIFU MFUMO WA CBMS ULIOBORESHWA ILI KUBORESHA USIMAMIZI WA BAJETI YA SERIKALI
Wataalam wa wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali wameagizwa kutumia mafunzo ya Mfumo ulioboreshwa wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS), kuboresha utendaji kazi katika usimamizi wa uandaaji na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali.
Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Kamshina wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye wakati akifungua mafunzo ya Mfumo wa CBMS ulioboreshwa na baadae kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2024/25, Maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/26 na kupata maoni ya kuboresha mchakato wa maandalizi ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/27.