WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UHUSIANO ULIOPO KATI YA WASHIRIKA NA SERIKALI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo endelevu. Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo ngazi ya Juu.