WASHIRIKA WA MAENDELEO KUCHANGIA SH. BILIONI 161 MFUKO WA AFYA WA PAMOJA

Serikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), wamesaini Hati ya makubaliano ya kuchangia katika Mfuko huo kiasi cha dola za Marekani milioni 55.86 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 161.33 kwa mwaka wa fedha 2025/26. Hafla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam kati ya Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, TAMISEMI na Wizara ya Afya na Washirika wa Maendeleo, wakishuhudiwa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange.