WASANII WATAKIWA KUWA MFANO KATIKA ELIMU YA FEDHA

Wasanii wanaoshiriki zoezi la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) lililopata semina ya elimu hiyo, wametakiwa kuwa mfano kwa jamii kwa kuzingatika sheria na kanuzi za uendeshaji wa shughuli za kutoa elimu ya huduma ndogo za fedha. Hayo yameelezwa mkoani Morogoro na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, wakati akifunga Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii TACCI, yaliolenga kutoa elimu ya fedha kwa njia bunifu ya sanaa.