WARATIBU HUDUMA NDOGO ZA FEDHA WAPIGWA MSASA

Serikali imeandaa mafunzo ya waratibu wa biashara ya huduma ndogo za fedha ili kuwajengea uwezo na kupata mrejesho wa utekelezaji wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na Kanuni zake za mwaka 2019. Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo jijini Dodoma, Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mkakati wa Serikali kuwajengea uwezo waratibu pamoja na kujadili changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa Sheria na Kanuni hizo na mapendekezo ya kukabiliana nazo.