WANANCHI WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali kwa kuwa mambo yote iliyoyapanga yatatekelezwa kikamilifu. Ametoa rai hiyo alipotembelea na kuzungumza na washiriki wa banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo. Dkt. Mwamba alisema katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyosomwa hivi karibuni, Serikali itahakikisha inatekelezwa kiufasaha na kufukia malengo yaliyo kusudiwa.