WANANCHI WAKARIBISHWA KUTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

Wananchi wamekaribishwa kutembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ili kupata elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara hiyo pamoja na baadhi ya taasisi zilizo chini yake. Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo alipotembela banda hilo na kuzungumza na waoneshaji kutoka Wizara na Taasisi zake. Alisema katika banda hilo wananchi watapata elimu kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali na uandaaji wake, sera mbalimbali za usimamizi wa kodi, usimamizi wa mali za Serikali, mifumo ya malipo na mishahara.