WANANCHI WA SIMIYU WATAKIWA KUTUMIA ELIMU YA FEDHA KUKUZA UCHUMI

Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya fedha kutoka kwa wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutumia elimu watakayoipata kukuza uchumi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Kenani Kihongosi, Ofisini kwake, alipotembelewa na Timu ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya wataalamu hao kuelekea Wilayani Itilima Mkoani Simiyu kutoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa Wilaya hiyo.