WANANCHI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA - SABASABA 2024
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Boniphace Kirindimo (Kulia), akimwelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, Prof. Geraldine Rasheli, namna ambavyo uandaaji wa bajeti ya Serikali unavyofanyika, wakati alipotembelea Banda la Wizara, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.