WAKANDARASI WA NDANI KUNUFAIKA NA MIRADI YA SERIKALI

Serikali imeweka kwenye Sheria kiwango cha thamani ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa na wazawa kutoka shilingi bilioni 10 hadi shilingi bilioni 50 ili kuwawezesha wazawa kunufaika na kuwafanya wawe walipakodi wakubwa kwa maendeleo ya nchi. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali, Makandarasi na Washauri Elekezi wa Ndani ulioangazia nafasi yao katika utekelezaji wa miradi.