WAJASIRILIAMALI WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA ELIMU YA UJASIRIAMALI

Wajasiriamali wa Kata ya Tutuo, Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora, wameiomba Serikali kuwapatia elimu ya ujasiriamali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora, ambazo zitakidhi ushindani wa soko ili kujikwamua kiuchumi. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Kata ya Tutuo, Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora, Bi. Doroth Mgombela, alipokutana na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambayo ilifika wilayani humo, kutoa elimu ya fedha kwa Wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya fedha kujikomboa kiuchumi.