WAJASIRIAMALI WADOGO WAPATA ELIMU YA FEDHA SUMBAWANGA
Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuwashauri wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika semina zinazoendelea kutolewa kuhusiana na elimu ya fedha ili kuepukana na mikopo umiza ama mikopo kausha damu.
Hayo yamesemwa na Bw. Salim Kimaro, Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, wakati wa Semina na Wajasiriamali wadogo iliyofanyika katika kumbi za Manispaa Wilaya ya Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa kwa kuwahimiza wananchi wote popote pale walipo waendelee kutufuatilia na kuhudhuria katika maeneo ambayo yatafanyika semina hizo ili waweze kujipatia elimu ya fedha kwa mustakabali wa uchumi wao na Taifa kwa ujumla.