WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO WAASWA KUTUMIA MAARIFA WALIYOPATA KUJIAJIRI
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula, amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kutumia elimu, maarifa na ujuzi walioupata kujiajiri, kuanzisha shughuli za kiuchumi na kuajiri wengine badala ya kutegemea ajira za kuajiriwa pekee.
Akiongea kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika Mahafali ya 40 ya Chuo Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Kampasi Kuu ya Dodoma, Mhe. Luswetula alisema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi, hususan vijana, kupata elimu, mitaji, teknolojia na masoko ili washiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
