WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU WASISITIZWA KUZINGATIA UADILIFU

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imehimizwa kuendelea kusisitiza wanachama wake umuhimu wa kuzingatia misingi ya uaminifu na uadilifu katika kazi zao za kila siku ili kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuongeza tija na ufanisi katika maendeleo ya nchi. Rai hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati wa Mahafali ya 47 ya Bodi hiyo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha APC-Mbweni, Dar es Salaam.