WADAU WAPITISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU SDGs

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha Tanzania inatimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDGs), ambayo pamoja na mambo mengine, yamelenga kuondoa umasikini katika jamii. Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua warsha ya wadau kwa ajili ya kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, kabla ya kuwasilishwa katika Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani Mwezi Julai, 2023.