VODACOM YAIPONGEZA SERIKALI KUONDOA TOZO ZA MIAMALA YA SIMU KWANI IMEKUZA BIASHARA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha sera za kodi ili kuchochea uwekezaji kutoka sekta binafsi ili kukuza uchumi wa nchi, ajira na maisha bora kwa watanzania. Dkt. Nchemba (Mb) amesema hayo Jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire.