VIWANGO VYA KUBADILISHA FEDHA VYAKUZA DENI NCHI ZA AFRIKA

Madeni ya nchi nyingi za Afrika yanakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa viwango vya riba na kubadilisha fedha duniani na kusababisha kushuka kwa thamani ya fedha za ndani. Hayo yamebainishwa Mjini Victoria Falls, Zimbabwe, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati wa Mkutano wa 56 wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi kutoka nchi za Umoja wa Afrika unaoratibiwa na Kamisheni ya Uchumi chini ya Umoja wa Mataifa (UNECA).