VIONGOZI WA WIZARA YA FEDHA WAWASILI OFISINI KUANZA KAZI BAADA YA KUAPISHWA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Elijah Mwandumbya, wakiwa wamekabidhiwa maua ya pongezi na watumishi wa Wizara hiyo, walipowasili katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, baada ya kuapishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiongoza Wizara hiyo.