VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NA WAFANYABIASHARA MTWARA WAPATIWA ELIMU YA FEDHA.

Vikundi vya Huduma ndogo za fedha pamoja na Wafanyabiashara mbalimbali kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani, wameshiriki katika mafunzo ya utunzaji fedha yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi za Fedha pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara, na kushirikisha wafanyabiashara na wananchi zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali.