VIJANA WATAKIWA KUPELEKA MALALAMIKO YA HUDUMA ZA FEDHA MAMLAKA HUSIKA
Vijana wametakiwa kuwasilisha malalamiko yao kuhusu huduma za fedha katika mamlaka husika ili kupata suluhu haraka pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Fedha ikiwemo utapeli, udanganyifu na mikopo yenye riba kubwa (mikopo umiza/ kausha damu).
Mamlaka wanazotakiwa kuwasilisha malalamiko hayo ni Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Dhamana ya Masoko na Mitaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima na Ofisi ya Waziri Mkuu.