USERIKALI: WEKEZAJI WA TWIGA CEMENT KWENYE KIWANDA CHA TANGA CEMENT KUONGEZA TIJA
SERIKALI imewahakikishia watanzania kuwa uwekezaji mpya wa zaidi ya dola za Marekani milioni 400 utakaofanywa na Kiwanda cha Saruji cha Twiga kwenye Kiwanda cha Saruji Tanga, utaongeza uzalishaji wa saruji, kukuza ajira na mapato ya Serikali kupitia kodi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), walipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda cha Tanga Cement, Jijini Dodoma.