UMAHIRI WA MAAFISA WAWAKOSHA VIONGOZI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA-SABASABA
Viongozi mbalimbali waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, wameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuwa na mikakati mizuri ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu Majukumu na Sera za Wizara Fedha, ili kuchochea maendeleo.
Baadhi ya viongozi waliotembelea Banda ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. Fransis Mwakapalila na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza.