TRADE MARK AFRIKA KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI NCHINI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El- maamry Mwamba. Mkutano huo umeidhinisha bajeti ya mwaka 2024/2025 kiasi cha dola za Marekani milion 7.1 ambayo itatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza ufanisi wa biashara nchini na ukanda kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa vijana na wanawake katika kufanya biashara hususan katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).