TANZANIA YASISITIZA MAPATO YA NDANI NA UBIA KATIKA UGHARIMIAJI WA MAENDELEO

Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesisitiza kuwa Tanzania imejikita katika kutumia mapato ya ndani kama kipaumbele cha kwanza katika kugharamia miradi ya maendeleo na mageuzi ya kiuchumi. Mheshimiwa Balozi Omar, amesema hayo wakati akiwasilisha ramani ya kiuchumi ya Tanzania katika Jukwaa la 25 la Kimataifa la Uchumi-Afrika-OECD, liliofanyika jijini Paris nchini Ufaransa, akiwa miongoni mwa wanajopo 7 walioalikwa rasmi kuwa wazungumzaji katika Jukwaa hilo.