TANZANIA YASHUKURU MCHANGO WA BENKI YA DUNIA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI TANZANIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo na Tanzania, hususan katika ufadhili wa miradi ya kimkakati, maendeleo ya rasilimali watu, nishati na miundombinu ya usafirishaji, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa. Ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Afrika la nchi wanachama wa Benki hiyo anayemaliza muda wake, Dkt. Zarau Kibwe, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Kundi la Benki ya Dunia, jijini Bangkok, Thailand.