TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA SITA (6) WA KAMATI MAALUM YA MAWAZIRI WA FEDHA, MIPANGO YA KIUCHUMI NA MTANGAMANO WA UMOJA WA AFRIKA.
Tanzania imeshiriki Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, uliobeba kaulimbiu ya “Afrika baada ya Majanga”: Majadiliano juu ya Uwekezaji, Ukuaji Endelevu wa Uchumi na Ustawi kwa wote”. Mkutano huo uliojumuisha nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, umefanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).